Ni muhimu kutunza vulva yako na uke wako (sehemu ya siri ya kike). Hali nyingi ambazo zinaathiri eneo hili ni kawaida na ni rahisi kutibu. Lakini ni muhimu kuzungumza na daktari wako ikiwa una wasiwasi.
Kuna tofauti gani na vulva yako na uke wako?
Watu wengine wanafikiri vulva na uke ni kitu kimoja - lakini ni tofauti. Vulva yako ni sehemu ya nje ya sehemu ya siri ya kike ambayo inaonekana. Inajumuisha:
- sehemu inayokuwa na mavuzi (nyewele ya mbeleni)
- midomo ya nje, ambayo imekuwa na nywele za sehemu ya siri (labia majora)
- midomo ya ndani, ambayo haikuwa na mavuzi (labia minora)
- kisimi na kifuniko chake
- ufunguzi wa mkojo (ambapo mkojo unatoka)
- ufunguzi wa uke.
Uke wako uko ndani mwili wako. Uke unaenea kutoka vulva yako kwenda kwa mwanzo wa mfuko wa uzazi. Uke wako upo ambapo hedhi yako hutiririka kutoka kwa mfuko wa uzazi, ambapo unaweza kupenya (k.m. ngono) na ambapo watoto hupitia wakati wa kuzaliwa.
Mchoro wa vulva na uke
Nini inaweza kuathiri eneo hili?
Mwasho
Ngozi ya uke wako ni dhaifu sana, kwa hivyo vitu vingi vinaweza kusababisha kuwasha.
Mwasho wa uke unaweza kusumbua. Dalili zinaweza kujumuisha:
- kuchoma au kujikuna
- hisia ya msisimko chini ya ngozi yako
- rangi ya nyekundu au uvimbe
- ufa au mpasuko wa ngozi
- ngozi ziwe nyeupe
- ngono yenye maumivu.
Utoko
Wanawake wote wana utoko wa uke na majimaji ambayo yanaweka uke na uke unyevu na afya. Lakini wakati mwingine utoko unasababishwa na maambukizi.
Maambukizi
Kuna maambukizi mbalimbali yanayoweza kuathirika vulva na uke, kwa mfano, ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani (thrush). Ugonjwa wa kuvimba ndani kwa ndani mwilini (thrush), unaosababishwa na Kandida, unaoathiri karibu 75% ya wanawake angalau mara moja katika maisha yao.
Maambukizi ya uke yanaweza kusababisha dalili kama vile:
- mchomo au mwasho karibu na ukeni
- utoko wa uke ambao una harafu au rangi tofauti kuliko ya kawaida
- hisia ya uchungu wakati wa kujisaidia
- uvimbe au rangi ya nyekundu wa vulva na uke
- mipasuko ya ngozi ya vulva (uke)
- ngono yenye maumivu.
Mzio na hali za ngozi
Baadhi ya bidhaa zinaweza kusababisha mwitiko wa mzio ambao ungeweza kuwasha vulva (uke) iwe rangi ya nyekundu. Kwa mfano, visodo (tampons), sabuni, suruali inayobana ya usanisi (Lycra) na klorini (kutoka mabwawa ya kuogelea). Kuna hali nyingine za ngozi zinazoweza kuathiri vulva (uke).
Kuzeeka
Wakati wa kukoma hedhi, ngozi zako za uke zinaweza kuwa nyembamba zaidi, kusababisha ukavu, mwasho na maumivu wakati wa ngono.
Maumivu ya uke
Maumivu ya uke yanaweza kusababishwa na mambo mbalimbali. Kwa mfano, maambukizi, hali za ngozi, kubana kwa misuli ya sakafu ya nyonga, uharibifu wa neva na uharibifu wa tishu kutokana na upasuaji au kujifungua.
Wakati wa kumwona daktari wako
Ni muhimu kumwona daktari wako ikiwa una wasiwasi kuhusu muwasho, utoko au maumivu ya uke.
Daktari wako huenda kufanya mtihani, uchunguzi au vipimo vingine ili kujua ni nini inayosababisha tatizo. Kulingana na sababu, anaweza kukupa marashi, krimu au vidonge. Aanaweza pia kutoa ushauri juu ya jinsi ya kutunza eneo hili. Katika baadhi ya visa, anaweza kukurejelea kwa mtaalamu.
Unaweza kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kutunza uke wako kwa kusoma kijitabu cha Jean Hailes 'The vulva’ (kupatikana katika Kiingereza pekee).
Ili kupata maelezo, nyenzo na marejeleo, tembelea kwa jeanhailes.org.au/health-a-z/vulva-vagina.
© 2024 Jean Hailes Foundation. All rights reserved. This publication may not be reproduced in whole or in part by any means without written permission of the copyright owner. Contact: licensing@jeanhailes.org.au